Mafundisho
Makini ya Biblia
Jifunze Neno la Mungu mtandaoni kwa muda wako, kupitia kozi mbalimbali za mafundisho ya Biblia yaliyokusudiwa kukujenga kiroho na kukupatia tumaini na mwanga mpya katika maisha yako.
Tuna kila unachohitaji ili
ukue katika Neno la Mungu
Masomo yaliyopangiliwa vyema
Endelea mbele hatua kwa hatua, kupitia kozi zetu za Biblia zilizoandaliwa Kitaalam katika Moduli, Masomo na vyanzo vya kutosha vitakavyokujenga kiroho.
Pima Maendeleo Yako Mwenyewe
Fanya tathmini baada ya kila somo na pokea matokeo yako mara moja.
Vyeti vinavyotambulika
Kamilisha kozi na upokee cheti cha PDF kinachoweza kupakuliwa ili kuthibitisha mafanikio yako katika kujifunza Biblia.
Dashibodi ya maendeleo
Ona masomo yaliyokamilika, maendeleo ya kozi, historia ya majaribio na vyeti vyako katika dashibodi moja ya mwanafunzi.
Huduma za kichungaji
Ukipenda waweza kushiriki nasi maamuzi yako ya kiroho na uunganishwe na mchungaji kwa maombi, mwongozo na hatua zinazoweza kuhitajika.
Mafundisho Mkononi Mwako
Jifunze popote kwa kutumia simu, tableti au kompyuta ukifurahi uzoefu uliosanifiwa vyema kwa kila skrini.
Sisi ni Jamii ya Waaminio tunaojengwa juu ya Neno la Mungu
Kuanzia wanafunzi wapya, mpaka kwa waumini wenye uzoefu, jukwaa hili linamkaribisha kila mtu anayetaka kuugundua na kuuelewa ukweli wa Biblia.
Unaweza kuanza kwa hatua hizi 4 rahisi
Hakuna ugumu wowote. Fungua tu Biblia yako na uanze.
Tengeneza akaunti
Jisajili bure ndani ya dakika chache na ujipatie dashibodi yako.
Chagua kozi
Tazama kozi za Biblia zilizopo na ujiunge kwa kubofya mara moja tu.
Anza Kozi
Kamilisha masomo yako kwa kasi uliyojipimia na pima uelewa wako kupitia majaribio.
Pata cheti
Maliza kozi na upakue cheti chako binafsi.
Kuna zaidi ya kujifunza:
Haya ni Maisha Yanayobadilishwa
Neno la Mungu linapougusa moyo wako, safari haikomei katika alama za majaribio. Shiriki maamuzi yako ya kiroho na uunganishwe kwa faragha na mtu atakayekulea kiroho.
Ushuhuda wa Wanafunzi Wetu
"Masomo haya yamenisaidia kuielewa Biblia kwa uwazi na kwa namna ya kuvutia. Hatimaye nimepata njia ya kujifunza ukweli kwa namna bora sana."
"Jukwaa hili linaonekana kuwa la kisasa na linaendana na wakati. Niliweza kujifunza kwenye simu, nimefanya majaribio na nimepokea huduma ya kichungaji kwa wakati nilipohitaji."
"Cheti kilinipatia hamasa ya kumaliza. Nilikishiriki na familia yangu na nimewahimiza na nao wao kuanza safari hii."
Tumaini halisi, Huanza na Ujuzi wa Neno
Jifunze Biblia, ukue kiroho na kuimarisha mahusiano yako na Mungu kwa kujifunza kile alichokusudia katika maisha yako kupitia Mafundisho ya Biblia yaliyo bora na yaliyo na ufasaha. .
Tunaamini katika Neno Tunakufikia Mkononi Mwako· na Tunapatikana Popote