Taswira ya Mafundisho Kuhusu Mungu (Teolojia)

Mafundisho Kuhusu Mungu (Teolojia)

Kozi hii inajenga uelewa na msingi wa kumjua Mungu kupitia njia mbalimbali alizotumia Mungu ili kumsaidia Mwanadamu kupata njia ya kuhusiana na Mungu.

Muundo wa kozi
MZB-101
Ngazi ya msingi
Credits 3
Muda wa kujifunza
Wiki 10
5 moduli / 21 masomo
Sharti la kufaulu
Pata Cheti Chako
Unahitaji kupata angalau asilimia 75% ili iweze kufaulu.
Matokeo ya kujifunza
  • Kueleza mamlaka ya Maandiko Matakatifu katika imani na maisha.
  • Kufafanua fundisho la Utatu Mtakatifu kwa msingi wa Biblia.
  • Kutambua kazi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu katika mpango wa wokovu.
  • Kuweka msingi imara wa kiteolojia kwa kozi nyingine zote zinazofuata.
Vitabu na miongozo
  • Biblia Takatifu
  • Imani za Msingi
  • Seventh-day Adventists Believe

Yaliyomo katika kozi

Hakuna kitabu ambacho kimepata kupendwa, kuchukiwa, kuhofiwa, kushutumiwa kama Biblia. Watu wamekufa kwa ajili ya Biblia. Wengine wameua kwa ajili yake. Imehamasisha matendo makubwa na ya maana ya mwanadamu, na imelaumiwa kwa matendo maovu ya wanadamu. Vita vimepiganwa kwa ajili ya Biblia, mapinduzi yamepangwa kwa kusoma kurasa zake ...

Rejea
Biblia Takatifu
  • Somo la 01: Msingi wa Maandiko Matakatifu
    Utangulizi • Ufunuo wa Mungu • Ufunuo wa kiujumla
    Dakika 30-40
  • Somo la 02: Ufafanuzi wa Maandiko Matakatifu
    Uandishi wa Biblia • Uvuvio wa Maandiko • Mchakato wa Uvuvio
    Dakika 40-50
  • Somo la 03: Maendeleo ya Maandiko Matakatifu
    Uvuvio na Historia • Usahihi wa Maandiko • Mamlaka ya Maandiko Matakatifu
    Dakika 30-40
  • Somo la 04: Matumizi ya Maandiko Matakatifu
    Yesu na Mamlaka ya Maandiko • Roho Mtakatifu na Mamlaka ya Biblia • Kiwango cha Mamlaka ya Maandiko Matakatifu
    Dakika 30-40
  • Somo la 05: Muhtasari wa Maandiko Matakatifu
    Dakika 10-15

Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, umoja wa Nafsi tatu za milele. Mungu asiyeweza kufikwa na mauti, mwenye enzi zote, mwenye uwezo wote, mwenye kujua yote, juu ya yote, na aliyepo daima. Hana kikomo na anapita ufahamu wa kibinadamu, walakini akijulikana kupitia ufunuo wake mwenyewe.

Rejea
Biblia Takatifu
  • Somo la 06: Msingi wa Utatu Mtakatifu
    Utangulizi • Mungu Aweza Kujulikana • Kupata Ufahamu wa Mungu
    Dakika 20-30
  • Somo la 07: Maendeleo ya Utatu Mtakatifu
    Ushahidi wa Maandiko Matakatifu • Mungu wa Maandiko Matakatifu • Matendo ya Mungu
    Dakika 40-50
  • Somo la 08: Matumizi ya Utatu Mtakatifu
    Uteule wa Asili na Uhuru wa Mwanadamu • Utendaji katika Utatu Mtakatifu • Mahusiano katika Utatu Mtakatifu
    Dakika 50-60
  • Somo la 09: Muhtasari wa Utatu Mtakatifu
    Dakika 10-15

Mungu Baba wa milele ni Mwumbaji, Chimbuko, Mtegemezaji, na Mfalme wa viumbe vyote. Ni mwenye haki na mtakatifu, mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na upendo na kweli. Tabia na uwezo vilivyoonyeshwa ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni ufunuo wa Baba.

Rejea
Biblia Takatifu
  • Somo la 10: Msingi wa Mungu Baba
    Utangulizi • Maoni juu ya Baba • Mungu wa Rehema
    Dakika 30-40
  • Somo la 11: Maendeleo ya Mungu Baba
    M ungu wa Kimbilio • M ungu wa Uaminifu • Mungu Baba Katika Agano Jipya
    Dakika 50-60
  • Somo la 12: Muhtasari wa Mungu Baba
    Dakika 10-15

Mungu Mwana wa milele alifanyika mwili katika Yesu Kristo. Katika Yeye vitu vyote viliumbwa, tabia ya Mungu imefunuliwa katika Yeye, wokovu wa jamii yote ya mwanadamu unakamilishwa na ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu aliye Kristo.

Rejea
Biblia Takatifu
  • Somo la 13: Mungu Mwana
    Utangulizi • Kufanyika Mwili – Utabiri na Utimilifu wake • Onyesho la Kiunabii la Wokovu
    Dakika 50-60
  • Somo la 14: Ufafanuzi wa Mungu Mwana
    Wakati wa Huduma yake na Kifo • Kufufuka kwa Mwokozi • Asili mbili za Yesu Kristo
    Dakika 50-60
  • Somo la 15: Maendeleo ya Mungu Mwana
    Yesu Kristo ni Mwanadamu kweli kweli. • Kiwango cha kujitambulisha kwake na asili ya Mwanadamu • Muungano wa Asili Mbili
    Dakika 50-60
  • Somo la 16: Matumizi ya Mungu Mwana
    Kristo ni Muungano wa Asili mbili • K uunganisha Asili Mbili • Umuhimu wa Kuunganisha Uungu na Uanadamu
    Dakika 40-50
  • Somo la 17: Muunganiko wa Mungu Mwana
    Vyeo vya Yesu Kristo • Kristo Nabii • Kristo Kuhani
    Dakika 50-60
  • Somo la 18: Muhtasari wa Mungu Mwana
    Dakika 10-15

Mungu Roho Mtakatifu wa milele alikuwa mtendani pamoja na Baba na Mwana katika Uumbaji, katika Yesu kufanyika mwili na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa Maandiko Matakatifu. Alijaza maisha ya Yesu Kristo na uwezo. Huwavuta na kuasadikisha wanadamu; na wale wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha akiwapatia maisha mapya.

Rejea
Biblia Takatifu
  • Somo la 19: Roho Mtakatifu
    Utangulizi • Roho Mtakatifu ni Nani? • Roho Mtakatifu Kwa Uhalisi ni Mungu
    Dakika 50-60
  • Somo la 20: Maendeleo ya Roho Mtakatifu
    Utume wa Roho Mtakatifu • Asili ya Utume • Hujaa kwenye mioyo ya Waumini
    Dakika 40-50
  • Somo la 21: Muhtasari wa Roho Mtakatifu
    Dakika 10-15
5 moduli 21 masomo
$0.00 $3.00
100% OFF Ofa Maalum
Inaisha 31 Jul 2026
Jisajili ili ujiunge Ingia
Kinachohitajika Ili Kujiunga

Kozi hii inafaa kwa kila mtu. Huhitajiki kozi yoyote kabla ya kujiandikisha — karibu ujiunga moja kwa moja!